About

SMV is a meat processing company that manufactures a variety of meat products located in Dar es Salaam. With animals raised at our own farms, we control the entire process from farm to plate. We are looking for passionate individuals to join our team to grow together.

Recommendations

Experience

Kampuni ya kuchakata na kusindika vyakula jijini Dar es Salaam inatafuta mtu mwenye uwezo, nia, na ari
ya kujiunga na timu yetu kama mchakataji wa nyama. Lengo letu ni kutengeneza nyakati za furaha katika
kila nyumba nchini Tanzania.


Muhtasari
Nafasi Iliyopo: Afisa Usindikaji wa Nyama Aina ya Ajira: ya Kudumu (kwa Mkataba)
Anaripoti kwa: Meneja Msaidizi Ratiba ya Kazi: Jumatatu-... Jumamosi
Malipo: Mshahara + NSSF + WCF + Chakula
Kama afisa usindikaji wa nyama, utawajibika na usindikaji wa nyama, kufungasha, na kutekeleza kazi
zinazohusisha utayarishaji wa nyama. Kazi inaweza kujumuisha kazi maalum za kuchinja, kukata nyama
kwa viwango tofauti, na kutengeneza bidhaa za nyama kama soseji.
Ofisi ipo Makumbusho au Mikocheni. Nafasi hii inahitaji kujituma nje ya masaa ya kawaida ya kazi.
Tafadhali usitume maombi ikiwa hauna shauku, utayari, na moyo wa kujituma kufanya kazi hii.


Ujuzi Unaohitajika
Awe na uwezo wa kuwasiliana (kwa maneno na maandishi) kwa Kiswahili; Kiingereza kitakuwa faida
zaidi
Kiwango cha chini cha elimu ya sekondari. Mafunzo ya ziada yatakuwa faida zaidi
Uzoefu wa kazini na mafunzo katika usindikaji wa nyama yatakuwa faida zaidi
Ujuzi mzuri wa utatuzi wa shida na mawasiliano ili kutatua changamoto katika kuchakata nyama
Uwezo wa kufanya kazi vizuri katika mazingira ya timu
Kuzingatia maelezo
Nguvu nzuri ya mwili, ukakamavu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira mbalimbali
Ujuzi au uwezi wa kutumia mashine na zana za kuchakata nyama


Majukumu Muhimu
Kukata na kuchakata nyama kulingana na matakwa ya wateja
Kutumia vifaa na machine za nyama kama mashine ya kukata na kusaga nyama
Kupima uzito na kufunga bidhaa za nyama kwa ajili ya kuuza na kusambaza
Kudumisha usafi wa vifaa na maeneo ya kazi
Kuhakikisha kuwa bidhaa za nyama zinashughulikiwa, kuhifadhiwa na kutayarishwa kulingana na
viwango na kanuni za usalama wa chakula
Kutoa huduma kwa wateja kwa kujibu maswali, kupokea maagizo na kutoa mapendekezo
Kudumisha hesabu sahihi na kuagiza vifaa kama inahitajika
Kutoa mafunzo na kusimamia wafanyakazi wengine kama inahitajika
MWISHO WA KUOMBA MAOMBI: 30 October, 2024
Tuma CV kwa au WhatsApp:
 more
  • Manufacturing
  • Nipo nimesoma food and beverage maana yake chakula na vinywaji nimefanya kazi new Africa otel miaka 8 kwa sasa nipo home my mobile phone ... +255717414199 +255787725211 email matokeompapi38@gmail.com najua lugha tatu kingereza kiswahili na french kifaransa asanteni jina langu MATOKEO EDWARD MPAPI  more